Katika kipindi cha uongozi wake, Mufti amefanikisha mambo makubwa ndani ya muda mfupi, kama vile: Kuunganisha Waislamu wote Tanzania bila kujali Madhehebu adhehebu yao, kwa kusisitiza kuwa wote ni wafuasi wa Mtume mmoja, Muhammad (saww), na Kusimamia na kulingania amani na maridhiano, ili kukuza mshikamano wa kitaifa na kuimarisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya Tanzania.

20 Septemba 2025 - 14:10

Waislamu nchini Tanzania Waadhimisha Miaka 10 ya Uongozi wa Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Dr. Abubakar Zubair bin Ally +Picha

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- limearifu kuwa leo, Ijumaa tarehe 19 Septemba 2025, Waislamu wa Tanzania wameadhimisha Miaka 10 ya Uongozi wa Mufti na Sheikh Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Sheikh Dr. Abubakar Zubair bin Ally. Siku hii imepewa jina la “Mufti Day”, ikiwa mahsusi kwa ajili ya kujadili maendeleo na mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha muongo mmoja wa uongozi wake.

Waislamu nchini Tanzania Waadhimisha Miaka 10 ya Uongozi wa Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Dr. Abubakar Zubair bin Ally +Picha

Wageni na Viongozi Waliohudhuria

Hafla hiyo imefanyika katika viwanja vya Makao Makuu ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) na kuhudhuriwa na viongozi wa Serikali, Masheikh na wageni mbalimbali akiwemo:

1_Mheshimiwa Abdallah Hamis Ulega, Waziri wa Ujenzi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - ambaye ndiye aliyekuwa Mgeni rasmi wa hafla.

2_Sheikh Dr. Alhad Mussa Salum, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT-TAIFA).

3_Dr. Maarefi, Mkurugenzi wa Kitengo cha Utamaduni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

4_Mheshimiwa Albert Chalamila, Mkuu wa Mkoa wa Dar-es-Salaam.

Na viongozi wengine mashuhuri wa kitaifa na kidini.

Waislamu nchini Tanzania Waadhimisha Miaka 10 ya Uongozi wa Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Dr. Abubakar Zubair bin Ally +Picha

Tuzo na Zawadi

Katika shamrashamra za tukio hilo, Mheshimiwa Mufti amekabidhiwa na kupokea zawadi pamoja na tuzo kutoka kwa Masheikh wa Mikoa yote ya Tanzania, ikiwa ni ishara ya heshima na kutambua mchango wake mkubwa katika dini na jamii.

Waislamu nchini Tanzania Waadhimisha Miaka 10 ya Uongozi wa Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Dr. Abubakar Zubair bin Ally +Picha

Maneno ya Mtume (s.a.w.w)

Hafla hii pia imeungwa mkono na kauli ya Mtume Muhammad (s a.w.w) isemayo:
"Na sema: Fanyeni Kazi, na Mwenyezi Mungu ataona Kazi yenu, na Mtume wake na Waumini."

Waislamu nchini Tanzania Waadhimisha Miaka 10 ya Uongozi wa Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Dr. Abubakar Zubair bin Ally +Picha

Mafanikio ya Mufti Dr. Abubakar Zubair

Katika kipindi cha uongozi wake, Mufti amefanikisha mambo makubwa ndani ya muda mfupi, ikiwemo:

1_Kuunganisha Waislamu wote Tanzania bila kujali Madhehebu adhehebu yao, kwa kusisitiza kuwa wote ni wafuasi wa Mtume mmoja, Muhammad (saww).

2_Kusimamia na kulingania amani na maridhiano, ili kukuza mshikamano wa kitaifa na kuimarisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya Tanzania.

Waislamu nchini Tanzania Waadhimisha Miaka 10 ya Uongozi wa Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Dr. Abubakar Zubair bin Ally +Picha

Your Comment

You are replying to: .
captcha